BUKOBA SPORTS

Thursday, December 12, 2013

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: DROO RAUNDI YA MTOANO TIMU 16 KUFANYIKA JUMATATU DESEMBA 16 HUKO NYON USWISI KUANZIA SAA 8 MCHANA. ARSENAL, CHELSEA, MAN CITY NA MAN UNITED ZA ENGLAND KUPANGWA NA NANI?

DROO ya UEFA CHAMPIONS LIGI, ili kupanga Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 itafanyika huko Nyon, Uswisi Jumatatu Desemba 16 kuanzia Saa 8 Mchana.
Katika Droo hiyo, Mabingwa Watetezi, Bayern Munich na Washindi wa Pili, Borussia Dortmund, wamo pamoja na wenzao wengine wawili wa Germany, Bayer Leverkusen na FC Schalke.
Ligi Kuu England inazo Timu 4 ambazo ni Mabingwa wake Manchester United, Man City, Chelsea na Arsenal. 

Real Madrid, ambao wanasaka Taji lao la 10 Ulaya, wamo pamoja wenzao wa Spain, Barcelona na Atletico Madrid.
Italy imebakiwa na Timu moja tu ambayo ni AC Milan.
Miongoni mwa Timu hizo 16 ambazo zimo kwenye Droo, 4 zimetokea kwenye Raundi za Awali za Mchujo za UCL Msimu huu.
Kwa mujibu wa Kanuni za Droo, Timu zitawekwa kwenye Vyungu viwili, Chungu Namba 1 ni wale Washindi wa Makundi na Chungu Namba 2 ni Washindi wa Pili wa Makundi.

Droo hii itaendeshwa na Katibu Mkuu wa UEFA, Gianni Infantino, na Mkurugenzi wa Mashindano wa UEFA, Giorgio Marchetti, wakisaidiwa na Balozi wa Fainali za UCL 2013/14, Gwiji Luis Figo.
Kitakacho zingatiwa ni kuwa Timu toka Chungu Namba 1 itapambanishwa na Timu toka Chungu Namba 2 isipokuwa Timu zilizotoka Kundi moja au Nchi moja hazitaruhusiwa kukutana.

Pia, Washindi wa Makundi wataanza Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 Ugenini hapo Februari 18/19 na 25/26 na kumalizia Nyumbani hapo Machi 11/12 na 18/19.
CHUNGU NA 1- WASHINDI WA MAKUNDI:
-Manchester United(England)
-Real Madrid CF (Spain)
-Paris Saint-Germain (France)
-FC Bayern München (Germany, Mabingwa Watetezi)
-Chelsea FC (England)
-Borussia Dortmund (Germany)
-Club Atlético de Madrid (Spain)
FC Barcelona (Spain)

CHUNGU NA 1- WASHINDI WA PILI WA MAKUNDI:
-Bayer 04 Leverkusen (Germany)
-Galatasaray AŞ (Turkey)
-Olympiacos FC (Greece)
-Manchester City FC (England)
-FC Schalke 04 (Germany)
-Arsenal FC (England)
-FC Zenit (Russia)
-AC Milan (Italy)

No comments:

Post a Comment