Katika Mechi ya Kwanza huko Nou Camp Wiki iliyopita, Barca iliichapa Real Sociedad Bao 2-0.
Kwenye Mechi ya Jana Usiku, Barca walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 27 la Lionel Messi na Real Sociedad kusawazisha katika Dakika ya 87 kwa Bao la Antoine Griezmann.
Juzi, kwenye Marudiano ya Nusu Fainali nyingine ya Kombe hili, Bao mbili za Cristiano Ronaldo ziliwabwaga nje waliokuwa Mabingwa Watetezi wa Kombe hili, Atletico Madrid, waliofungwa 2-0 na Real Madrid na kutolewa kwa Jumla ya Bao 5-0 kwani walichapwa 3-0 huko Santiago Bernabeu katika Mechi ya Kwanza Wiki iliyopita.
Fainali itachezwa hapo Aprili 19 katika Uwanja utakaotangazwa baadae.
NUSU FAINALI/MATOKEO
Marudiano
Jumanne Februari 11
Atletico de Madrid 0 v Real Madrid CF 2 [0-5]
Jumatano Februari 12
Real Sociedad 1 v FC Barcelona 1 [1-3]
FAINALI
Aprili 19
Real Madrid v Barcelona
No comments:
Post a Comment