Kipindi cha kwanza dakika ya 17 Atletico Madrid wamejifunga bao kupitia kwa mchezaji wao Emiliano Insua na kufanya Real waitangulie kwa bao hilo kipindi cha kwanza kwa kumalizika kwa bao 1-0, Kipindi cha pili dakika ya 57 Jese Rodriguez amewapatia bao la pili na kufanya 2-0 Atletico Madrid.
Jese Rodriguez akishangilia bao lake dakika ya 57 kipindi cha pili.
Wachezaji wa Real Madrid wakishangilia bao lao la kwanza
Cristiano Ronaldo akijaribu kumtoka mchezaji wa Atletico de Madrid usiku huu
Dakika ya 73 kipindi cha pili Atletico Madrid wakajifunga tena bao safi kwa kupitia mchezaji Miranda. Bao hilo la kujifunga kwa Miranda limehitimisha jumla ya bao 3-0 na mpira kumalizika huku kocha wao Atletico Madrid Diego Simeone akipewa kadi ya njano.
Zinedine Zidane nae alikuwemo uwanjani kuwacheki Real Madrid
Kocha Diego Simeone amepewa kadi ya njano kwenye mtanange huu.
COPA del REY
NUSU FAINALI
Marudiano
Jumanne Februari 11
23:00 Atletico de Madrid v Real Madrid CF [Estadio Vicente Calderon]
Jumatano Februari 12
24:00 Real Sociedad v FC Barcelona [Estadio Anoeta]
FAINALI
Aprili 19
No comments:
Post a Comment