BUKOBA SPORTS

Friday, February 14, 2014

DAYNA NYANGE NA CINDY SANYU WA UGANDA WAKUTANA JIJINI MWANZA LEO! USIKU HUU HAPATOSHI NDANI YA UKUMBI WA JB BELMONTE HOTEL (SERENGETI HALL) HAPA MWANZA. VALENTINE DAY YA LEO NI BALAA!!!

Msanii wa muziki wa bongo fleva Dayna Nyange mwenye maskani yake mjini Morogoro,ambaye pia ni msanii pekee wa kike anafanya vizuri kutoka Morogoro leo usiku atakuwa kwenye jukwaa moja na msanii wa muziki Cindy Sanyu kutoka Nchini Uganda katika usiku wa wapendanao (Valentine Day) leo Ijumaa katika Ukumbi wa JB Belmonte Hotel (Serengeti Hall). Wasanii hawa wawili hawatakuwa wao peke yao pia kutakuwepo na wasanii wengine kama Zedy Y, K Fan, Dogo D, na Mwanza Rainbow Dancers.
Msanii wa muziki wa bongo fleva Dayna Nyange (kulia) akiwa na Msanii mwenzake kutoka Nchini Uganda Cindy Sanyu leo katika ukumbi wa JB Belmonte Hotel wa jijini Mwanza. Tayari kwa kutoa Burudani kali leo siku ya wapendanao (Valentine Day 2014). Msanii Cindy Sanyu kutoka uganda (kushoto) katikati ni Promota wao Bw. Baraka Nyororo na kulia ni msanii wa Bongo Flava wa hapa Nchini Tz Dayna Nyange.
Cindy Sanyu na Dayna Katika picha ya Pamoja.
Hakika siku ya leo itakuwa haitoshi!! itakuwa Valentine Day ya aina yake hapa JB Belmonte Hotel Mwanza.
Picha ya wasanii na Promota wao.

No comments:

Post a Comment