KITUO cha redio Kasibante fm Bukoba leo Ijumaa kitasherehekea siku ya wapendanao (Valentine day) na Watoto Yatima wa hapa Bukoba kutoka katika vituo mbalimbali vyakulelea watoto wasio jiweza hapa Bukoba.
Uongozi wa redio hiyo pia umeandaa hafla hiyo ikiwa ni pamoja na kufurahia kiujumla siku hii ya wapenda nao na kuwataka wazazi na walezi wa waishio mjini hapa Bukoba na sehemu mbali mbali kujitokeza katika siku ya leo Ijumaa katika eneo hilo kuwasaidia watoto hao Yatima. www.bukobasports.com ikiongea na mmoja wa wafakazi hapo amesema kuwa kutakuepo na zawadi mbalimbali ikiwemo Vitabu, Madaftari na kalamu, Nguo nk. vitatolewa kwa wototo. Pia uongozi utashiriki katika Chakula cha mchana pamoja na watoto hao, Lengo ni kuunganisha watoto hao kujiona na wao ni Binadamu kama wengine na kupata Upendo kutoka kwa Wazazi na kujiona hawajatengwa.

Sisi wote ni ndugu!!

Baadhi ya Wafanyakazi wa Radio Kasibante Fm. kushoto ni Abdulzack na Jerome.
No comments:
Post a Comment