BUKOBA SPORTS

Friday, February 7, 2014

KOCHA MANUEL PELLEGRINI NA WINGER WA SUNDERLAND ADAM JOHNSON WAPEWA TUZO YA MWEZI JANUARI.

MANUEL PELLEGRINI na ADAM JOHNSON ndio waliosomba Tuzo za Januari kwa kuwa Bora kwa Mwezi Januari kwa Ligi Kuu England.
Bosi wa Manchester City, Manuel Pellegrini, ametwaa Tuzo ya Meneja Bora na Winga wa Sunderland, Adam Johnson, ndie Mchezaji Bora.
Kwa Pellegrini, hii ni Tuzo ya Pili mfululizo kutwaa kwani Mwezi Desemba yeye pia alikuwa ndie Meneja Bora.

Manchester City, chini ya Manuel Pellegrini, walishinda Mechi zao zote 4 kwa kuzifunga Ugenini Swansea, Newcastle na Tottenham na kuifunga Nyumbani Cardiff City Bao 4-2 na hivi sasa wako Nafasi ya Pili, Pointi 2 nyuma ya Vinara Arsenal.

Nae Adam Johnson ameshinda Tuzo hii kwa kuweza kuifungia Sunderland Bao 5 ikiwemo Hetitriki walipoichapa Fulham.

Hapo Jana, Wadhamini wa Ligi Kuu England, Barclays, walitoa Listi ya Wagombea Tuzo kwa Mwezi Januari na Gus Poyet, Jose Mourinho, Manuel Pellegrini na Tony Pulis waliteuliwa kuwania Tuzo ya Barclays ya Meneja Bora.
Kwa Mwezi Januari walioteuliwa kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora walikuwa ni Yaya Toure, Adam Johnson, Santi Cazorla na Luis Suarez.



WASHINDI WALIOPITA MSIMU 2013/14:
December
Player: Luis Suarez (Liverpool); Manager: Manuel Pellegrini (Manchester City)
November
Player: Tim Krul; Manager: Alan Pardew (both Newcastle United)
October
Player: Sergio Aguero (Man City); Manager: Mauricio Pochettino (Southampton)
September
Player: Aaron Ramsey; Manager: Arsene Wenger (both Arsenal)
August
Player: Daniel Sturridge; Manager: Brendan Rodgers (both Liverpool).


Manager to have won the Manager of the Month award twice in a row
Joe Kinnear , Wimbledon, Mar/Apr 1994
Kevin Keegan, Newcastle, Aug, Sep 1995
Roy Evans , Liverpool, Dec, Jan 1995/96
Sir Alex Ferguson , Manchester United, Feb/Mar 1996, Mar/Apr 2000
Arsene Wenger , Arsenal, Mar/Apr 1998
David O'Leary , Leeds, Mar/Apr 2001
Paul Jewell , Wigan, Sep/Oct 2005
Rafa Benitez , Liverpool, Nov/Dec 2005
Carlo Ancelotti , Chelsea, Mar/Apr 2011
Manuel Pellegrini, Manchester City, Dec/Jan 2013/14

No comments:

Post a Comment