
Msimu wa Man United ulizidi kudidimia Jumanne Usiku wakati walipofungwa 2-0 huko Ugiriki na Olympiacos katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
Ukichukulia Man United, ambao ndio Mabingwa Watetezi, wapo Pointi 11 nyuma ya Timu ya 4 kwenye Ligi Kuu England na wapo Pointi 15 nyuma ya Vinara Chelsea, baadhi ya Watu wamedai Moyes yupo njiani kupigwa Buti.
Lakini Robin van Persie amemtetea Moyes kwa kusema: “Yeye ni mpya na anahitaji muda. Anafanya bidii pamoja na sisi. Ni rahisi kumyooshea kidole Meneja lakini ni sisi tunatakiwa kuleta mafanikio Uwanjani.”
Licha ya kukiri huu ni Msimu mbovu kwao, Robin van Persie amesisitiza kuwa upo uwezekano mkubwa wa kuwabwaga Olympiacos katika Mechi ya Marudiano Old Trafford hapo Machi 19.
"We are lousy - in a lousy position in the league, out of the cups and this looks a difficult one also"
Robin van Persie
No comments:
Post a Comment