Campbell ambaye ni mshindi mara mbili wa Olimpiki katika mbio za mita 200 alishinda rufaa aliyowakilisha katika mahakama kuu ya Rufaa katika michezo Duniani CAS.
Campebell ambaye amekuwa akisisitiza kuwa hakuwahi tumia dawa hiyo iliyopigwa marufuku na anasema alifedheheshwa sana na matukio yaliyomnyima fursa ya Kutetea taji lake la mita mia mbili la dunia mwaka uliopita .
Campbell anatarajiwa kuiwakilisha Jamaica katika mashindano ya ndani yatakayoandaliwa huko Poland mwezi ujao na Labda mashindano ya Jumuiya ya Madola yatakayofanyika mwezi Julai .
No comments:
Post a Comment