Rais wa timu hiyo, Athuman Mohamed akiwa na mmoja wa raia wa Comoro aliyekwenda kuilaki timu hiyo.
Na Richard Mwaikenda
TIMU ya Comorozine ya Comoro, imetamba kuifumua Yanga mabao 2 -0 katika mechi itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kesho kutwa na katika mechi ya marudiano nyumbani kwao wameapa kuifundisha adabu timu hiyo ya mitaa ya Jangwani na Twiga mabao 5-0, katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Tambo hizo zilitolewa na Rais wa timu hiyo, Athuman Mohamed wakati tiku hiyo ilipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam jana usiku kwa ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATC).
Alisema kuwa timu yake imejiandaa vizuri kukabiliana na Yanga na kwamba kilichowaleta Tanzania ni kusaka ushindi tu, si vinginevyo.
Timu hiyo, iliyokuja na jumla ya wachezaji 20 na viongozi tisa ilipokelewa na Ofisa Itifaki wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Raphael Matola na Bernard Mwalala kwa niaba ya Yanga.
Mohamed alisema kuwa wachezaji wanaowahofia sana katika kikosi cha Yanga ni Mrisho Ngassa na Emmanuel Okwi ambaye hata hivyo hawajui kama mchezaji huyo hatacheza mechi hiyo kutokana na katazo la Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (FIFA).
Timu hiyo ya Comorozine ambao ni mabingwa wa Kisiwa cha Comoro, wamefikia katika Hoteli ya Surphers Dar es Salaam.
Timu ya Yanga imeweka kambi yake Bagamoyo kujiandaa na mechi hiyo muhimu.
mwisho
No comments:
Post a Comment