BUKOBA SPORTS

Thursday, March 6, 2014

CAF CHAMPIONZ LIGI: AL AHLY v YANGA SASA KUCHEZWA ALEXANDRIA JUMAPILI HII TAREHE 9 MARCH. UWANJA WA EL-HEDOUD KUTUMIKA!!

CHAMA cha Soka cha Egypt, EFA, kimetangaza kuwa Mechi ya Marudiano ya Raundi ya Kwanza ya CAF CHAMPIONZ LIGI kati ya Al Ahly na Yanga itachezwa Harras El-Hedoud Stadium Mjini Alexandria hapo Jumapili.
Kabla ya tamko hilo kumekuwa na kutokujua wapi pambano hilo muhimu litachezwa baada Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri kukataza pambano hilo kuchezwa Mjini Cairo baada Mashabiki wa Al Ahly wenye msimamo mkali, Ultra Ahlwy, kutamka watahudhuria Mechi hiyo licha ya Mashabiki kukatazwa kuingia ndani ya Uwanja.

Baada ya hapo Maafisa wa Al Ahly walianza kuhaha kutafuta Uwanja mwingine na kuamua Mechi ichezwe huko El Gouna Stadium kwenye Mji mdogo wa El Gouna lakini Kocha Mkuu na Wachezaji wa Al Ahly walipinga uamuzi huo.

Akitangaza Mechi hii kuhamishiwa huko Harras El-Hedoud Stadium Mjini Alexandria na kuchezwa Jumapili, Mkurugenzi wa EFA, Tharwat Suweilem, amesema: “Mechi itachezwa huko Alexandria na Wizara ya Mambo ya Ndani imetutumia Barua rasmi ya kuhakikisha usalama na sisi tumeipeleka Barua hiyo kwa CAF na Yanga.”
Nae Kiongozi wa Al Ahly, Sayed Abdul Hafez, anadaiwa kuzungumza na Viongozi wa Yanga waliokuweko huko Cairo ili wakubali Gemu ichezwe huko Alexandria baada Jana kutoa msimamo wao kuwa hawakubali ichezwe nje ya Cairo.

Katika Mechi ya Kwanza, Al Ahly, ambao ndio Mabingwa Watetezi wa CAF CHAMPIONS LIGI, walifungwa Bao 1-0 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Wiki iliyopita kwa Bao lilofungwa na Nadir Haroub "Cannavaro".

No comments:

Post a Comment