BUKOBA SPORTS

Thursday, March 6, 2014

TASWIRA KADHAA ZA JIJI LA WINDHOEK NAMIBIA

Namibia ni moja ya nchi zilizopo Kusini mwa Afrika ikiwa na idadi ya watu wapatao2,113,077 hii ni kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2011. Namibia iliyopata uhuru wake Machi 21, 1990 na kabla ya hapo ilikuwa ikujulikana kama German South-West Africa.

Namibia imepakana na Bahari ya Atlantiki katika mpaka wake wa Magharibu na Pia inapakana na Nchi za Zambia na Angola kwa upande wa Kaskazini na Mashariki inapakana na nchi za Afrika Kusini na Bostwana.
Nchi ya Nabibia inategemea sana uchumi wake kutoka katika Sekta ya Madini ambayo inachangia Uchumi wa taifa kwa asilimia 10.4, Kilimo ni asilimia 5 na Viwanda ni asilimia 13.5 pamoja na utalii, lakini pia inapata mgao kutoka Afrika Kusini kutokana na nchi hiyo kuitawala kwa muda mrefu.


Namibia inamiundombinu mizuri sana ya barabara na hakika imejipanga sawasawa.

Hii ni barabara inayotokea Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako na maeneo mengine ya Namibia.


Mji ni msafi na kila mwendo mfupi kuna mapipa ya taka.

Barabara za juu na chini zimejengwa ili kukabiliana na foleni isiyokuwa na mpago.

Usafiri mkubwa wa mjini hapo ni Taxi ambazo hufanya kazi kama daladala kwa kubeba abiria mtaani.

Foleni haipo kabisa katikati ya mji kwa muda wote na marachache eneleo la viwandani huwa na folenbi kama hivi katika taa.

Huu ndo mji wa Windhoek Namibia.

No comments:

Post a Comment