BAO la Dakika za Majeruhi la Mchezaji alietoka Benchi,Panduleni “Kaka” Nekundi, limeiokoa Namibia na kuipa Sare ya Bao 1-1 walipocheza na Taifa Stars, Timu ya Taifa ya Tanzania.
Nae Mchezaji alietoka Benchi, Mcha Khamis, aliifungia Taifa Stars Bao Dakika 3 kabla Mpira kumalizika kufuatia Kona lakini Nekundi alifunga kwa Kichwa baada ya Frikiki iliyopigwa na Petrus Shitembi Dakika 5 ndani ya Dakika za Majeruhi.
Mechi hii ilishuhudiwa na Watu wasiozidi 2000 kwenye Uwanja wa Sam Nujoma na Watazamaji hao hawakuwa na furaha yeyote baada ya Timu yao kushindwa kutengeneza nafasi yeyote ya kufunga.
No comments:
Post a Comment