BUKOBA SPORTS

Friday, March 28, 2014

‘CLASS OF 92’: GARY & PHIL NEVILLE, GIGGS, SCHOLES & NICKY BUTT, WAKUBALIANA DILI KUINUNUA KLABU SALFORD CITY!

WACHEZAJI NGULI wa Manchester United, Gary Neville, Phil Neville, Ryan Giggs, Paul Scholes na Nicky Butt wamefikia makubaliano kuinunua Klabu ya Salford City.
Dili hiyo inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Msimu baada ya kupata baraka za FA, Chama cha Soka England na Wasimamizi wa Ligi.

Salford City ipo kwenye Ligi ya Evo-Stik Daraja la Kwanza huko Kaskazini mwa England Maeneo ya Jiji la Manchester na Uwanja wake upo Moor Lane huko Kersal.
Wachezaji hao wa zamani wa Man United wote chimbuko lao ni Maeneo ilipo Salford City.

Hivi sasa Ryan Giggs ni Kocha Mchezaji wa Man United, Phil Neville ni Kocha Msaidizi Man United chini ya David Moyes, Nicky Butt anafundisha Timu ya Vijana ya Man United wakati Gary Neville ni Kocha Msaidizi wa Timu ya Taifa ya England na pia ni Mchambuzi wa Soka kwenye Kituo cha TV cha Sky Sports.

Wakiongea kuhusu Salford City Wachezaji hao walitamka vitu mbalimbali na Gary Neville alisema: “Nilifanya majaribio yagu ya kwanza na Manchester United huko Salford nikiwa na Miaka 11 na sitasahau umuhimu wake!”
Paul Scholes amesema: “Tunajua ni ngumu lakini tuna nia na tuna plani nyingi hapo!”
Butt amesema: “Eneo hilo lina historia ya Miaka 320 nyuma na ni lazima lilindwe!”
Late? Giggs then had to run to make the meeting with Neville and Nicky Butt
Phil Neville: "Ni muhimu kulinda kazi ngumu iliyofanyika kwenye Ligi za chini!”
Giggs said: "Kila Mtu anajua umuhimu wa Salford kwangu mimi!”
Snap: Giggs has sealed a deal with Neville and stopped to pose a photo with a passer-by on Thursday
Nae Mwenyekiti wa Salford City, Karen Baird, amesema huu ni wakati wa furaha kwao kwani utaleta mafanikio makubwa kwao.
Akithibitisha Dili hii kwenye Mtandao wa Twitter, Gary Neville, aliwahakikishia Wadau kuwa Dili hiyo haimanishi kubadilishwa Jina Salford City wala Uwanja wake wala Menejimenti yake kama ilivyokuwa hulka ya Siku hizi kwa Wamiliki wapya wa Klabu
Fresh faced: (From left) Coach Eric Harrison with the Class of 92, Ryan Giggs, Nicky Butt, David Beckham, Gary Neville, Phil Neville, Paul Scholes and Terry CookeEnzi hizo!!! Eric Harrison na Giggs, Butt, David Beckham, Gary Neville, Phil Neville, Scholes pamoja na Terry Cooke

SALFORD CITY FC
Nickname: The Ammies
League: Evo-stick North League Premier
Ground: Moor Lane (cap 625 seated)
Manager: Barry Massey & Phil Power
Chairman: Karen Baird
Colours: Orange

No comments:

Post a Comment