KIUNGO wa Arsenal, Jack Wilshere, atakuwa nje ya Uwanja kwa Wiki 6 baada Mfupa wa Mguu wake wa Kushoto kupata ufa.
Wilshere, Miaka 22, aliumizwa na Daniel Agger wa Liverpool katika Dakika ya 12 kwenye Mechi iliyochezwa Jumatano Usiku Uwanjani Wembley wakati England ilipoifunga Denmark 1-0 katika Mechi ya Kirafiki.
Lakini Kiungo huyo aliendelea kucheza hadi Dakika ya 59 alipopumzishwa na baada ya Mechi alipimwa na kuonekana hakuumia sana.
Hii Leo, aliporudi Klabuni kwao Arsenal na kupimwa zaidi ikagundulika Mfupa wa Juu ya Vidole vya Mguu wake wa Kushoto una ufa.
Habari hii ni mbaya kwa Arsenal ambayo inakabiliwa na kipindi kigumu na Wilshere ataikosa Mechi ya Robo Fainali ya FA CUP Jumamosi watakapocheza na Everton na kufuatia Jumanne watakapokuwa huko Munich kurudiana na Bayern Munich kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI.
Baada ya Mechi hizo Arsenal wataenda White Hart Lane kucheza Dabi ya London ya Kaskazini dhidi ya Tottenham kwenye Mechi muhimu ya Ligi Kuu England.
MITANANGE YOTE HII KUIKOSA!!
March 8 Everton (H)
FA Cup Sixth Round
March 11 Bayern Munich (A)
UEFA Champions League Last 16, second leg
March 16 Tottenham (A)
March 22 Chelsea (A)
March 25 Swansea City (H)
March 29 Manchester City (H)
April 6 Everton (A)
April 13 West Ham (H)

No comments:
Post a Comment