BUKOBA SPORTS

Thursday, March 6, 2014

JOSE MOURINHO: WACHEZAJI WA MADRID NI SHIDA TUPU!! WANAJALI ZAIDI MUONEKANO WAO KULIKO KUSHINDA VIKOMBE!

MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amewaponda wachezaji wa Real Madrid kuwa anadhani wanajali zaidi muonekano wao kwa watu kuliko kushinda mataji. Mourinho aliondoka Madrid kwenda Chelsea mwaka jana baada ya kukaa Santiago Bernabeu kwa miaka mitatu na kudai alikuwa hafurahishwi na tabia zilizokuwa zikionyeshwa na wachezaji wakati akiwa huko.  ocha huyo amesema mara nyingi wachezaji wa Madrid walikuwa wakijipanga mbele ya kioo kabla ya mchezo wakati mwamuzi akiwasubiria koridoni lakini anadhani ndivyo jamii ya sasa ilivyo kwamba vijana wanajali zaidi mambo hayo. Mourinho amesema ameanza kazi ya ukocha mwaka 2000 na anadhani kipindi cha nyuma wachezaji walikuwa wakipigana kutengeneza fedha wakati wakicheza soka na kuwa matajiri baada ya kuachana na mchezo huo. Lakini hivi sasa watu wanaowazunguka ndio wanajaribu kuwafanya matajiri kabla hata hawajaanza kucheza soka.

No comments:

Post a Comment