BUKOBA SPORTS

Monday, March 3, 2014

KIKOSI CHA TAIFA STARS CHATUA WINDHOEK

Kikosi cha Taifa Stars kimeondoka leo alfajiri kwenda Windhoek, Namibia kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya wenyeji itakayochezwa Machi 5 mwaka huu.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ina msafara wa watu 25 unaoongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Timu imefikia hoteli ya Safari jijini humo.

Mechi hiyo itachezwa kwenye Uwanja wa Sam Nujoma, na kikosi cha Taifa Stars kipo chini ya Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi ambaye ana leseni A ya ukocha inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Namibia (Brave Warriors) inayofundishwa na kocha Ricardo Mannetti imeingia kambini jana (Machi 2 mwaka huu) kwa ajili ya mechi hiyo ambayo tiketi zake zilianza kuuzwa Februari 28 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment