BUKOBA SPORTS

Monday, March 3, 2014

LA LIGA: BARCELONA 4 v ALMERIA 1, SANCHEZ, MESSI, PUYOL NA XAVI WATINGISHA VYAVU, BARCA WAJIKITA NAFASI YA PILI!

Bao za Alexis Sanchez, Lione Messi, kwa Frikiki safi, Carles Puyol na Xavi, ziliwapa Barcelona ushindi wa Bao 4-1 walipocheza na UD Almeria Uwanjani Nou Camp katika Mechi ya La Liga na kuipiku Atletico Madrid na kushika Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 1 nyuma ya Vinara Real Madrid.

Bao hilo la Messi kwenye Mechi hii limemfanya afikishe Bao 229 kwenye La Liga na kumpita Nguli Raul, aliekuwa Nafasi ya 3, katika Ufungaji Bora wa La Liga katika Historia.
Kwenye Mechi hii, Kocha wa Barca, Gerardo Martino, alibadilisha Wachezaji 6 toka Kikosi kilichopigwa 3-1 na Real Sociedad Wiki iliyopita na Mchezaji mashuhuri aliepoteza Namba ni Andres Iniesta.Kikosi kilichoanza za Barca
UD Almeria
Nipishe!
Messi akiwaendesha UD Almeria
Neymar akituliza.

Neymar kwenye patashika.
Wachezaji wa Barca wakipongezana baada ya kupata bao jingine la tatu
Asante Messi!!
Kushinda ni kawaida yetu!!
Carles Puyol dakika ya 83 aliziona nyavu..
Hakunaga!!!

Xavi nae akaziona dakika za majeruhi dakika ya 89. 
LA LIGA:
MATOKEO:
Jumapili Machi 2

Villarreal CF 1 v Real Betis 1
Atletico de Madrid 2 v Real Madrid CF 2
Sevilla FC 1 v Real Sociedad 0
FC Barcelona 4 v UD Almeria 1
Rayo Vallecano 1 v Valencia 0

No comments:

Post a Comment