BUKOBA SPORTS

Saturday, March 1, 2014

HULL CITY 1 v NEWCASTLE UNITED 4, ALAN PARDEW AMTWANGA KICHWA MCHEZAJI DAVID MEYLER! NEWCASTLE WAIBUKA NA USHINDI MNENE!

Newcastle, wakicheza Ugenini, wameichapa Hull City kwao Bao 4-1 lakini Vichwa vya Habari ni kitendo cha Meneja wao Alan Pardew kumtwanga kichwa Mchezaji wa Hull, David Meyler, baada ya Mchezaji huyo kumsukuma wakati akifuata Mpira wa Kurusha.

Newcastle waliongoza 2-0 hadi Mapumziko kwa Bao za Moussa Sissoko na Loic Remy.
Curtis Davies aliifungia Hull Bao 1 mara baada ya Haftaimu lakini Moussa Sissoko akapachika Bao la 3 na kuifanya Newcastle iongoze Bao 3-1 na ndipo likaja tukio la Alan Pardew kumtwanga kichwa David Meyler ambalo lilimfanya Refa amtoe nje Meneja huyo.
Clashing point: David Meyler had to restrained by fellow player Hull City player Elmohamady
Newcastle wakapiga Bao lao la 4 kupitia Anita.
Patashika kati ya mchezaji na Kocha wa Newcastle Pardew na mchezaji David Meyler
Kocha wa Newcastle Pardew na mchezaji David Meyler wakizozana na kutupiana maneno ya hapa na pale!!!Kutoelewana!!! Vurugu zikiendelea....Majanga!!Kocha wa Newcastle Pardew na mchezaji David Meyler wakipelekeshana!!!
Kocha wa Newcastle Pardew na mchezaji David Meyle wakiamuliwa na Mwamuzi Howard Webb.

No comments:

Post a Comment