BUKOBA SPORTS

Monday, March 10, 2014

NANI MKALI? WASANII WA BUKOBA MJINI WAANZA MCHAKATO WA KUMCHAGUA MKALI WAO. MCHUANO UKISHIKA KASI..

Majaji, (kushoto) ni Jaji Merina N. Katambe na (kulia) ni Jani Optat Henry
Mchakato wa Wasanii wa Maigizo Bukoba unaendelea kushika kazi katika Mji wa Bukoba. Wasanii wakiendelea kuoneshana ubabe wa Kuigiza na hatimae kumpata mmoja Mkali ziadi. Jumapili 9, March 2014 Ulifanyika Mchujo wa kuwapata wasanii wa kusonga mbele kwa wale walifanya Vizuri na wengine walipunguzwa na Majaji katika Ufukwe wa Ziwa Victoria pande za Kiroyera Beach. Majaji wote wanafanya kazi zao vyema na wamesisita kuwa hakuna upendeleo wowote ule ni kujituma na kuonesha Kile kinachoelimisha na kuwafunza Wananchi na Jamii kujumla. Na Hatimae kumpata mkali wa wote.
Taswira, Majaji, (Kushoto) ni jaji Newton Kataraia, Merina N. Katambe, Optat Henry na wa mwisho ni Shadrack Kalekayo. Hapa kalamu zilikuwa zikifanya kazi kutoa pointi na kwa waliochemka kuambiwa wazi wazi katika Shindano hili la kumtafuta mkali wa Kuigiza hapa Bukoba Mjini.
Taswira katikati ni Msanii Onyango akionesha Usanii wake mbele Majaji na Watazamaji katika fukwe za ziwa Victoria pande za Kiroyera Beach.
Vijana wakiwaangalia wasanii wakiendelea na kuigiza..
Jaji Optat  Henry (kulia) akifurahia baada ya kumuona msanii Teso Boy alivyoingia tu uwanjani..
Dada nao hawakuwa nyuma!!
Msanii Teso Boy

Msanii wa Maigizo Bukoba Teso Boy akionesha kipaji chake mbele ya Umati wa Watu wengi walikujitokeza kwa wingi katika ufukwe wa Ziwa Victoria pande za Kiroyera Beach.

Wadau wa Maigizo Bukoba wakiwacheki wenzao Uwanjani

Jaji Bi. Merina N. Katambe akitoa neno
Msanii wa Kuigiza Bw. Teso Boy
Bw. Willy Kiroyera Mgombea Uwenyekiti wa KRFA nae alikuwepo mahala hapa kuwaona vijana wakichuana.


Huyu nae...Mganga wa Kienyeji...

Kuigiza si kazi ndogo!!! Jamii lazima uioneshe kile wanachojielimisha!!!
Chezea Mganga wewe!!!

Kuigiza siyo mchezo.....Mvuvi kaibiwa pochi yake ...nini kinafata baada ya kumpata kibaka!!
Watoto, Vijana, Wazee wote walikusanyika mahala hapa kuwacheki wasanii wao wa Bukoba Mjini kile wanachosikia na hapa walijionea wazi.
Kiroyera Beach....palikuwa hapatoshi!!!

No comments:

Post a Comment