BUKOBA SPORTS

Sunday, March 9, 2014

TAIFA STARS KUTUMIA UZI WA ADIDAS


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilifikia makubaliano na kampuni ya Adidas kupitia msaada wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kupatiwa vifaa vya michezo.

Kufuatia makubaliano hayo TFF tulipatiwa vifaa kadhaa vya adiads kwa ajili ya timu ya Taifa ya wakubwa (Taifa Stars). Vifaa hivyo zikiwemo jezi tulianza kuvitumia kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Namibia iliyochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek kama inavyoonekana pichani. 
Vifaa hivyo zikiwemo jezi vitaendelea kutumiwa na Taifa Stars hadi hapo utaratibu mpya wa jezi za timu ya Taifa utakapokamilika.
TFF Tunawashukuru Adidas ambao ni washirika wa CAF na Shirikisho la Kimataifa la mpira wa Miguu (FIFA) wa miaka mingi na kuendeleza swala zima la mpira wa Miguu hapa Nchini.

No comments:

Post a Comment