BUKOBA SPORTS

Tuesday, March 4, 2014

TFF KUWAADHIBU WAWILI TWIGA STARS KUTOKANA NA ULEVI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatafakari hatua zaidi za kinidhamu dhidi ya wachezaji wawili wa kikosi cha Twiga Stars walioondolewa kwenye timu hiyo na Kocha Rogasian Kaijage.

Kocha Kaijage aliwatimua kambini wachezaji Mwapewa Mtumwa na Flora Kayanda kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu wakati Twiga Stars ikijiandaa kwa mechi ya marudiano ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Zambia.

Twiga Stars ilipoteza mechi ya kwanza ugenini mabao 2-1 na kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya marudiano iliyochezwa Februari 28 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex, hivyo kutolewa katika mashindano hayo kwa jumla ya mabao 3-2.

TFF tunaunga mkono hatua iliyochukuliwa na Kocha Kaijage dhidi ya wachezaji hao wakongwe wa Twiga Stars, kwani katika shughuli yoyote ile inayohitaji ufanisi nidhamu ni kitu cha kwanza.

Twiga Stars itacheza mechi za mchujo za michezo ya 11 ya Afrika (All Africa Games) ambayo itafanyika mwakani nchini Congo Brazzaville.

No comments:

Post a Comment