BUKOBA SPORTS

Wednesday, April 23, 2014

DAVID MOYES KULIPWA FIDIA YA PAUNDI MILLIONI 5 BAADA YA KUTIMULIWA

David Moyes atalipwa fidia ya £5million baada ya kufukuzwa kazi na Manchester United – ikiwa ni kipengele cha makubaliano ya mkataba wake na klabu hiyo.
Kocha huyo wa zamani wa Everton amekaa miezi 10 tu katika mkataba wake wa miaka 6 na, hatua hiyo imekuja baada ya kuwa na mfululizo mbaya wa matokeo. Katika mkataba wa Moyes na United kulikuwa na kipengele kinachoeleza ikiwa Manchester United ingefeli kufuzu kucheza Champions League msimu huu basi ikatokea United wakaamua kusitisha mkataba wake basi fidia isingezidi mshahara wake wa miezi 12 ambao ni £5million.Ryan Giggs ndie anashikilia nafasi yake mpaka mwisho wa msimu huu.David Moyes akiteta jambo na Ryan Giggskipindi cha nyuma kidogo ambapo Giggs ndie amepangwa kushika nafasi iliyoachwa na kocha huyo tangu jana.

No comments:

Post a Comment