BUKOBA SPORTS

Sunday, April 13, 2014

FULL TIME - LIVERPOOL 3 v MANCHESTER CITY 2, MAJOGOO LIVERPOOL WAPETA KILELENI!! PHILIPPE COUTINHO AKIWAPACHIKIA BAO LA USHINDI!


Mpira umeanza.....
Kipindi cha kwanza....
  Raheem Sterling anaipachikia bao dakika ya 6 Liverpool baada 
        ya kupata pasi kutoka kwa Luis Suárez. 

Dakika ya 26 Martin Skrtel anaipachikia bao lingine la pili kwa kichwa baada ya kona kupigwa na Steven Gerrard. 
 Kipindi cha pili dakika ya 57 David Silva alianza kusawazisha kwa kufanya 2-1.
 Dakika ya 63 kipindi cha pili Glen Johnson wa Liverpool alijifunga bao na kufanya 2-2. 
 Dakika ya 78 Philippe Coutinho akaiwasha bao lingine la tatu baada ya beki wa City Vincent Kompany kufanya makosa kutoa pasi hewa kwa kumgawia adui, Bao ni 3-2. 
-Jordan Henderson anapewa kadi nyekundu baada ya kumfanyia rafu mbaya Nasri katika dakika za majeruhi...Full Time!!!
Martin Skrtel akifunga bao la kichwa la pili baada ya kupokea kona iliyipigwa na Steven Gerrard na kuunganisha kwa staili ya aina yake na kuweka 2-0 dhidi ya Manchester City.Skrtel akipongezana na Kapteni wa Liverpool Steven Gerrard baada ya bao kupatikana.
VIKOSI:Liverpool: Mignolet, Johnson, Skrtel, Sakho, Flanagan, Henderson, Gerrard, Coutinho, Sterling, Suarez, Sturridge.
Subs: Brad Jones, Toure, Agger, Aspas, Moses, Lucas, Allen.

Man City: Hart, Zabaleta, Kompany, Demichelis, Clichy, Toure, Fernandinho, Jesus Navas, Silva, Nasri, Dzeko.
Subs: Lescott, Milner, Negredo, Kolarov, Javi Garcia, Aguero, Pantilimon.
Mapokezi ya timu yao Liverpool kwenye uwanja wa Anfield

No comments:

Post a Comment