BUKOBA SPORTS

Wednesday, April 2, 2014

MECHI YA AZAM FC NA RUVU SHOOTING MLANDIZI YASOGEZWA MBELE!!

MCHEZO wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Azam FC na wenyeji Ruvu Shooting uliokuwa ufanyike Aprili6, mwaka huu Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani umesogezwa mbele hadi Aprili 9, imefahamika.

Wachezaji wa Ruvu Shooting wakifanya mazoezi
Ruvu Shooting Mechi yao ya mwisho kabla ya kukutana na Azam Fc walikuwa ni Kagera Sugar, Mchezo uliochezewa Kaitaba na kutoka sare ya kutofungana ya 0-0.

Ruvu Shooting kwenye msimamo wapo nafasi ya 8 wakiwa na pointi 29

Katibuwa Azam FC, Nassor Idrisa ‘Father’ ameiambia tovuti ya klabu kwamba, sababu za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)kuusogeza mbele mchezo huo ni Azam FC kuwa na wachezaji wengi katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini yaumri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes.
Ngorongoro Heroes inatarajiwa kuondoka kesho nchini kwenda Nairobi,Kenya kwa ajili ya mechi ya kuwania kucheza Fainali za Vijana Afrika, itakayochezwa Jumapili ya Aprili 6mwaka huu Uwanja wa Machakos ulioko kilometa 80 kutoka jijini Nairobi na Azam ina wachezaji zaidi ya watanokwenye kikosi hicho. Hao ni Aishi Manula, Bryson Raphael, Gardiel Michael, Kevin Friday, Mudathir Yahya, FaridMussa na Hamad Juma. Wachezaji waliobaki wa Azam FC wanaendelea na mazoezi Uwanja wa Azam Complex,Chamazi Dar es Salaam. Azam FC inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 53 baada ya kucheza mechi 23, ikifuatiwa naYanga SC yenye pointi 46 za mechi 22 na Mbeya City yenye pointi 45 za mechi 23.
CHANZO: TOVUTI YA AZAM

No comments:

Post a Comment