BUKOBA SPORTS

Wednesday, April 23, 2014

MKOA WA KAGERA WAKAMILISHA MAANDALIZI YA UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA MWAKA 2014


Mkoa wa Kagera unaendelea kukamilisha maandalizi ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa utakaofanyika Mei 2, 2014 katika Uwanja wa Kaitaba Manispaa ya Bukoba kuanzia saa 1: 00 asubuhi na kuendelea.
Katika kuhakikisha kila shughuli iliyopangwa siku ya uzinduzi inafanyika kama ambavyo imepangwa Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Bw. Nassor Mnambila ametembelea uwanja wa Kaitaba uliofanyiwa marekebisho makubwa na kujionea Halaiki ya watoto iinavyoendelea na mazoezi yake.


Katika kutembelea uwanja huo Bw. Mnambila, zilifanyika shughuli zote zitakazofanyika siku hiyo ya uzinduzi hasa watoto wa halaiki kuimba na kuonyesha vitendo kwa kuumba maneno mbalimbali na mfano wa Mwenge wa Uhuru ili kuhakikisha muda unazingatiwa siku ya uzinduzi.

Aidha Bw. Mnambila alitoa taarifa fupi kwa waandishi wa habari kuhusu maandalizi yalipofikia hivi sasa kwa kusema kuwa maandalizi hayo mpaka yanaendelea vizuri na yamegawanyika katika sehemu kuu nne ambazo ni Kama ifuatavyo.

Kwanza ni Marekebisho ya Uwanja wa Kaitaba ambao umefanyiwa marekebisho makubwa ya ujenzi wa vyoo vipya viwili, kurudisha mfumo wa maji, kuezeka majukwaa ya pembeni matatu na kurekebisha viti vyake, Kupakaa rangi na kuzungushia uzio mpya wa ndani, kazi ambazo zipo katika hatua za mwisho kabisa.


Pili, Halaiki ya watoto, Bw. Mnambila aliwajulisha Waandishi wa Habari kuwa watoto wa Halaiki kwa hivi sasa wameishaiva kupitia walimu wao na kinachosubiriwa ni siku yenyewe ya uzinduzi aidha bado wanaendelea kufanya mazoezi ili kujiimarisha vizuri zaidi.

Tatu ni Wageni waalikwa ambapo alisema kuwa wageni wa Kimataifa, Kitaifa na Mkoa tayari wamepelekewa mialiko ya kushiriki uzinduzi huo ili wahudhurie na kushiriki na wananchi wa Mkoa wa Kagera siku ya tarehe 2/05/2014


Nne Bw. Mnambila aliwashukuru Wadau, Watu binafsi, Taasisi mbalimbali, Wabunge na wananchi wote ambao waliombwa na kutoamichango yao kuchangia uzinduzi huo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2014.

Mwisho kabisa Katibu Tawala wa Mkoa wa KageraBw. Mnambira aliwaomba wananchi wa mkoa wa Kagera kuhudhuria kwa wingi siku ya Uzinduzi ili kushiriki pamoja katika tukio la kihistoria kwa Mkoa wa wetu Kuzindua Mbioa za Mwenge wa Uhuru Kitaifa


Imeandaliwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2014

No comments:

Post a Comment