Januzaj, mwenye Miaka 19, alizaliwa Mji Mkuu wa Belgium, Brussels, lakini kutokana na mizizi ya Wazazi wake alikuwa huru kuzichezea Nchi za Kosovo, Albania, Turkey na Serbia, lakini mwenyewe akaamua kuiwakilicha Belgium.
Januzaj ni mmoja wa Wachezaji 12 wanaocheza Soka lao kwenye Ligi Kuu England ambao wamo kwenye Kikosi hicho.
Chipukizi huyo alijiunga na Man United Mwaka 2011 na alikuwa Benchi kwenye Mechi ya mwisho ya Ligi Msimu uliopita, Mechi ambayo ndiyo pia ilikuwa ya mwisho kwa Meneja aliestaafu, Sir Alex Ferguson, ambayo Man United walitoka 5-5 na WBA.
Msimu huu, Januzaj ameichezea Man United Mechi 27 za Ligi.
Huko Brazil, Belgium wapo KUNDI B pamoja na watacheza Mechi ya Kwanza hapo Juni 17 dhidi ya Algeria, kisha Russia hapo Juni 22 na South Korea hapo Juni 26.
KIKOSI KIZIMA
Goalkeepers: Thibaut Courtois, Simon Mignolet, Koen Casteels, Silvio Proto
Defenders: Toby Alderweireld, Anthony Vanden Borre, Laurent Ciman, Vincent Kompany, Daniel van Buyten, Thomas Vermaelen, Nicolas Lombaerts, Jan Vertonghen
Midfielders: Axel Witsel, Steven Defour, Marouane Fellaini, Moussa Dembélé, Nacer Chadli, Kevin De Bruyne, Eden Hazard, Dries Mertens, Kevin Mirallas, Adnan Januzaj
Attackers: Romelu Lukaku, Divock Origi.
Reserves: Nainggolan, Pocognoli, Hazard, Gillet, Batshuayi, Van Damme
No comments:
Post a Comment