BUKOBA SPORTS

Sunday, May 25, 2014

CAF CHAMPIONS LIGI: TP MAZEMBE 1 v 0 AS VITA CLUB, SAMATTA AFANYA KWELI AFUNGA BAO LA PEKEE NA KUIPA USHINDI.

MBWANA SAMATTA, Straika mahiri wa Tanzania, Jioni hii huko Stade TP Mazembe, Lubumbashi, Congo DR, alifunga Bao pekee katika Dakika ya 62 wakati Tmu yake TP Mazembe ilipoitungua AS Vita Club, pia ya Congo DR, Bao 1-0 katika Mechi ya KUNDI A la CAF CHAMPIONS LIGI. 
Hizi ni Mechi za Pili kwa kila Timu katika Kundi lao na katika Mechi ya Kwanza, TP Mazembe ilifungwa Bao 1-0 na Al Hilal huko Sudan na AS Vita Club kuichapa Al Zamalek ya Misri Bao 2-1 walipocheza Mjini Kinshasa.
Hapo Jana, kwenye Mechi nyingine ya KUNDI A, Al Zamalek iliichapa A l Hilal ya Sudan Bao 2-1.

TP Mazembe na AS Vita Club ni Timu zenye upinzani mkali mno Nchini Congo DR ambao ulipelekea Watu 15 kufa Uwanjani walipokutana huko Kinshasa Wiki kadhaa nyuma wakati Mazembe ikishinda Bao 1-0 kwenye Mechi ya Ligi.

CAF CHAMPIONS LIGI
Makundi yapo mawili ya Timu 4 kila moja na watacheza mtindo wa Ligi, Nyumbani na Ugenini, ili kupata Timu mbili za juu toka kila Kundi kucheza Nusu Fainali.


RATIBA/MATOKEO:
Ijumaa Mei 16
Al-Hilal – Sudan 1 TP Mazembe - Congo, DR 0
Jumamosi Mei 17
Espérance Sportive de Tunis – Tunisia 1 Entente Sportive de Sétif – Algeria 2
Jumapili Mei 18
AS Vita Club - Congo, DR 2 Al Zamalek – Egypt 1
Club Sportif Sfaxien – Tunisia 5 Al Ahli - Benghazi - Libya 1
Jumamosi Mei 24
Al Zamalek – Egypt 2 Al-Hilal – Sudan 1 
Al Ahli - Benghazi – Libya 3 Espérance Sportive de Tunis – Tunisia 2
Jumapili Mei 25
TP Mazembe - Congo, DR 1 AS Vita Club - Congo, DR 0 
22:30 Entente Sportive de Sétif - Algeria v Club Sportif Sfaxien - Tunisia
Jumamosi Juni 7
3:00   Espérance Sportive de Tunis – Tunisia v- Club Sportif Sfaxien - Tunisia
3:00   Al-Hilal – Sudan v AS Vita Club - Congo, DR
3:00   TP Mazembe - Congo, DR v Al Zamalek - Egypt
CAF Kombe la Shirikisho
Makundi yapo mawili ya Timu 4 kila moja na watacheza mtindo wa Ligi, Nyumbani na Ugenini, ili kupata Timu mbili za juu toka kila Kundi kucheza Nusu Fainali.
Mechi za Kwanza
Jumamosi Mei 17
AS Real Bamako 1 ASEC Mimosa 1
AC Leopards v Coton Sport
Jumamosi Mei 24
Coton Sport 0 AS Real Bamako 0
ASEC Mimosa 0 AC Leopards 0
Mechi za Kwanza
Jumamosi Mei 17
Sewe Sport 1 Etoile du Sahel 1
Al Ahly 2 Nkana FC 0
Jumamosi Mei 24
Nkana 1 Sewe Sport 1
ES Sahel v Al Ahly

No comments:

Post a Comment