Akiwa Kambini na Timu ya Taifa ya England, Welbeck amesema: “Nataka nicheze katikati. Nimekuwa nikichezeshwa pembeni kushoto na sasa ni wakati nicheze Sentafowadi!”
Hata hivyo matakwa ya Welbeck huenda yakagonga mwamba kwani upo ushindani mkubwa kutoka kwa Robin van Persie na Wayne Rooney, pia Javier Hernandez ‘Chicharito’, na hata pengine akitua Straika mpya, huku Edinson Cavani wa Paris St-Germain, akitajwatajwa.
Welbeck, mwenye Miaka 23, amefafanua zaidi shida yake kwa kudai kwenye Mfumo wa 4-4-2, akichezeshwa pembeni kushoto, hulazimika pia kusaidi kwenye Difensi kwani yeye pia ni mmoja wa hao Viungo wanne na hivyo hupunguza nafasi zake za kufunga lakini kwenye Mfumo wa 4-3-3 huwa nafuu kwani yeye huwa Mshambuliaji tu na rahisi kuingia kati na kujaribu kufunga.
Amesema: “Inategemea Mfumo upi tunatumia, kwenye 4-4-2, inabidi uwe na kazi ya ziada ya pia kucheza Difensi lakini 4-3-3, nikiwa pembeni kushoto, inakuwa nafuu kwani nashambulia tu na naingia kati kwenye nafasi za kufunga!”
Hata hivyo, Welbeck amesema yeye anataka apewe nafasi zaidi: “Ule wakati wa Krismas nilipata nafasi nyingi kucheza na nilifunga Bao nyingi tu. Ninachotaka ni nafasi za kucheza!”
Welbeck alianzia kucheza Man United tangu akiwa Mtoto na kujiunga rasmi na Timu hiyo Mwaka 2007 na kuanza kuichezea Timu ya Kwanza Msimu wa 2011/12.
No comments:
Post a Comment