Bondia Said Mbelwa kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Karama Nyilawila wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa UBO uliofanyika katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam hata hivyo mshindi ajapatikana kutokana na fujo zilizotokea katika raundi ya nane
Bondia Zumba Kukwe kushoto akioneshana umwamba na Josef Njelekela wakati wa mpambano wao waliotoka droo
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimpongeza khalid chokolaa baada ya kuibuka mshindi katika mpambano wake
Na Mwandishi Wetu
MPAMBANO wa ubingwa wa UBO umekosa kutangazwa mshindi mbele ya mashabiki baada ya vurugu kubwa kutokea katika ukumbi wa Friends Corner Manzese Dar es salaam jana.
uUingwa huo uliokuwa ukigombaniwa na mabondia Said Mbelwa na Karama Nyilawila alishindikana kupatikana mshindi baada ya raundi ya nane bondia Karama kumpiga kichwa Mbelwa cha wazawazi na kusababisha Mbelwa kuhamaki kwa kulipiza kisasi na kumsukuma nje pia kumrukia wakati alipotoka nje ya ulingoni mpambano huo wa raundi kumi ulijikuta ukishia kwa raundi nane Waamuzi pamoja na majaji walikimbia ukumbini wakiwaacha mashabiki bila kuleta majibu ya mpambano huo hata hivyo Mbelwa alirudi ulingoni kwa ajili ya kuendelea kupambana na mpinzani waka alikimbia moja kwa moja kutokana na kuona ngumi za mtaani ndizo zinashika kasi.
wakati huohuo bondia Mada Maugo alimpiga mwenzake Thomas Mashali kwa ngumi tatu mfululizo
bila kufata sheria ambapo ni kinyume na taratibu za mchezo wa masumbwi duniani. Mabondia hao wote walionekana wamelewa walishindwa kuelewana mbele ya promota Ally Mwazoa
Katika mapambano ya utangulizi yaliyochezwa bondia Khalid Chokoraa ambaye ni mwanamuziki alimpiga kwa KO ya raundi ya kwanza Abdul Manyenza na Mwaite Juma alimpiga Athumani Rashid wa Tanga kwa pointi wakati Selemani Galile alipigwa kwa pointi na Abdalah Pazi
No comments:
Post a Comment