HAPA NA PALE, KWENYE TETESI...ADAM LALLANA KWENDA LIVERPOOL, LUKE SHAW KUTUA MAN UNITED!
KIUNGO wa Southampton, Adam Lallana, mwenye Miaka 26, na mwenzake Fulbeki Luke Shaw, Miaka 18, ambao wote wameteuliwa Kikosi cha Wachezaji 23 cha England kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil, inasemekana wako mbioni kuhamia Liverpool na Manchester United.
Inasadikiwa Liverpool imeshatoa Ofa kumnunua Lallana na Man United wamebwaga Dau la Pauni Milioni 27 kumnasa Shaw.
Mwenyekiti wa Southampton, Ralph Krueger, ameshasema kwamba Mastaa wao wako mbioni kuhamia Klabu Vigogo za England na wao wapo wazi kuzungumza na yeyote yule.
No comments:
Post a Comment