Man United walimaliza Msimu huu Nafasi ya 7 na hivyo kukosa kuwemo UEFA CHAMPIONS LIGI na EUROPA LIGI kwa Msimu ujao na hii ni mara ya kwanza tangu Msimu wa 1989/90 kwa Old Trafford kuzikosa Mechi za Ulaya.
Ingawa Giggs, ambae ni Meneja wa Muda wa Man United, amekiri hilo litaathiri sana Wachezaji wasiokuwa na Namba kwenye Timu kwa kukosa Mechi nyingi za kucheza, amebainisha kuwa pengine hiyo ni baraka kwao kwa kucheza Mechi chache Msimu huo mpya na hivyo kujiimarisha na kunufaika kwenye Ligi kama walivyonufaika Liverpool Msimu huu.
Giggs amesema: “Unaweza kutazama hilo kwa namna tofauti. Tuna Kikosi kikubwa na baadhi ya Wachezaji wanaweza kukosa nafasi za kucheza kama tupo nje ya Ulaya lakini ikiwa tutafanikiwa kwenda mbali kwenye Vikombe vya England hilo litawasaidia!”
No comments:
Post a Comment