
Jumamosii inatarajiwa kumalizika kwa kishindo huko Nou Camp wakati Barcelona watakapo wakaribisha Vinara Arletico Madrid kwenye Mechi ambayo itaamua nani Bingwa Msimu huu.
Hivi sasa, kukiwa bado Mechi moja tu, Atletico wako mbele ya Barcelona kwa Pointi 3 na Sare kwao katika Mechi yao hii kutawapa Ubingwa Atletico lakini ikiwa Barca watashinda basi watafungana kwa Pointi na Barca watapewa Ubingwa kwa kuwa na Matokeo Bora ya Uso kwa Uso kati yao kwa vile Timu hizi zilitoka 0-0 katika Mechi ya Kwanza huko Vicente Calderon.
Ni mara mbili tu katika Historia ya La Liga Bingwa amepatikana baada Timu mbili kufungana kwa Pointi na Ubingwa kuamuliwa kwa kutazama Matokeo ya Uso kwa Uso kati ya Timu hizo mbili.
Hali hii ya Bingwa kupatikana kwa Matokeo ya Uso kwa Uso ilitokea Msimu wa 1950/51 wakati Atletico walipowapiku Sevilla na mara nyingine ilikuwa ni Miaka 5 kabla ya hapo.
Hadi Wikiendi iliyopita, Vigogo wengine wa Spain, Real Madrid, walikuwemo kwenye kinyang’anyiro lakini wakapoteza mwelekeo baada kufungwa na Celta Vigo.
Barcelona, ambao ndio Mabingwa Watetezi, wao wanasaka Taji lao la 5 la Ubingwa ndani ya Miaka 6 iliyopita.
Ikiwa Atletico watatwaa Ubingwa wao watakuwa Klabu ya kwanza, mbali ya Real na Barca, kutwaa Ubingwa tangu Valencia wafanye hivyo Mwaka 2004.
Atletico na Barca zimekutana mara 5 Msimu huu
Msimu ulipoanza tu, kwenye Super Cup, Timu hizi zilitoka 1-1 huko Vicente Calderon na 0-0 kwenye Marudiano huko Nou Camp na Barca kutwaa Kombe kwa Goli la Ugenini.
Mwezi Januari, huko Vicente Calderon, Aletico na Barca zilitoka 0-0 kwenye La Liga.
Kwenye Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI, Mwezi Aprili, Atletico na Barca zilitoka 1-1 Nou Camp na Atletico kushinda 1-0 kwao Vicente Calderon.


LA LIGA: RATIBAMechi za mwisho
Ijumaa Mei 16
22:00 Malaga CF v Levante
Jumamosii Mei 17
17:00 Real Madrid CF v RCD Espanyol
19:00 FC Barcelona v Atletico de Madrid
23:00 Valencia v Celta de Vigo
Jumapili Mei 18
13:00 Real Sociedad v Villarreal CF
19:00 Osasuna v Real Betis
19:00 Rayo Vallecano v Getafe CF
19:00 Real Valladolid v Granada CF
19:00 UD Almeria v Athletic de Bilbao
22:00 Sevilla FC v Elche CF



The Brazilians inviting the Chilean to come join them






Stop cheating on Leo with Adriano, Ney!






VAMOS TEA
Mwezi Januari, huko Vicente Calderon, Aletico na Barca zilitoka 0-0 kwenye La Liga.
Kwenye Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI, Mwezi Aprili, Atletico na Barca zilitoka 1-1 Nou Camp na Atletico kushinda 1-0 kwao Vicente Calderon.
LA LIGA: RATIBAMechi za mwisho
Ijumaa Mei 16
22:00 Malaga CF v Levante
Jumamosii Mei 17
17:00 Real Madrid CF v RCD Espanyol
19:00 FC Barcelona v Atletico de Madrid
23:00 Valencia v Celta de Vigo
Jumapili Mei 18
13:00 Real Sociedad v Villarreal CF
19:00 Osasuna v Real Betis
19:00 Rayo Vallecano v Getafe CF
19:00 Real Valladolid v Granada CF
19:00 UD Almeria v Athletic de Bilbao
22:00 Sevilla FC v Elche CF
The Brazilians inviting the Chilean to come join them
Stop cheating on Leo with Adriano, Ney!
VAMOS TEA
No comments:
Post a Comment