BUKOBA SPORTS

Tuesday, May 13, 2014

LUIS SUAREZ NA TONY PULIS WATEULIWA KUTWAA TUZO LIGI KUU ENGLAND!

STRAIKA wa Liverpool Luis Suarez ametwaa Tuzo ya Barclay ya Mchezaji wa Msimu na Tony Pulis kutwaa ile ya upande wa Mameneja.
Barclay ndio Wadhamini wa Ligi Kuu England.
Suarez, mwenye Miaka 27, amefunga Bao 31 katika Mechi 33 za Ligi na kuisaidia Liverpool kumaliza Nafasi ya Pili kwenye Ligi Kuu England.
Mbali ya kutwaa Buti ya Dhahabu kwa kuwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu England, Suarez pia alitwaa Tuzo mbili za Mchezaji Bora wa Mwaka toka kwa PFA, Chama cha Wachezaji wa Kulipwa Soka England, na ile ya FWA, Chama cha Wanahabri wa Soka.

Nae Tony Pulis, mwenye Miaka 56, alitwaa wadhifa wa Meneja Klabuni Crystal Palace Mwezi Novemba na kuiwezesha Timu ipande kutoka Nafasi ya 19 na kumaliza Nafasi ya 11 kwenye Ligi Kuu England na hilo limemfanya atwae Tuzo ya Barclay ya Meneja Bora wa Msimu.

No comments:

Post a Comment