BUKOBA SPORTS

Thursday, May 1, 2014

OSE MOURINHO: PENATI YA DIEGO COSTA ‘IMETUUA’

MENEJA wa Chelsea, Jose Mourinho, anaamini Penati ya Kipindi cha Pili ya Atletico Madrid ndio iliyobadilisha Gemu yote baada Timu yake Jumatano Usiku kufungwa 3-1 Uwanjani kwao Stamford Bridge kwenye Mechi ya Pili ya Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI na Atletico kutinga Fainali.
Hadi Dakika ya 60, Gemu ilikuwa 1-1 lakini Samuel Eto’o, alieingizwa toka Benchi, alimchezea Faulo Diego Costa na ikatolewa Penati ambayo alipiga mwenyewe Straika huyo hatari na kufanya Bao ziwe 2-1. 
Sasa Atletico watacheza Fainali na Mahasimu wao wakubwa, Real Madrid, huko Estádio da Luz, Lisbon, Portugal hapo Tarehe 24 Mei 2014.
Mourinho amedai Goli hilo ndilo liliwamaliza kwani hadi wakati huo wao ndio walikuwa juu na kuikontroli Gemu.Amesema: “Mpaka Penati hiyo wao hawakuwa Timu Bora. Mpaka kabla Penati, sisi tulikuwa na Gemu mkononi, tulitawala, tulikuwa na nafasi nyingi. Tulifunga Bao safi lakini tuliruhusu Bao la kizembe. Tulijua kwenye Mipira iliyokufa tulikuwa na nafasi. Kichwa cha John Terry kilikuwa safi sana na Kipa aliokoa kiajabu na baada ya hapo Penati ikatuua. Ilibaki Timu moja tu. Ukweli ni kuwa kuanzia pale tulipoteza Gemu.”Hii ni mara ya 4 kwa Jose Mourinho kutolewa kwenye Nusu Fainali na sasa kuibakisha Timu yake ya sasa Chelsea ikiwa mikono mitupu Msimu huu na ikibakiwa na nafasi finyu kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England.

No comments:

Post a Comment