
Ikiwa imebaki siku moja kufika ziara ya uhamasishaji wa tuzo za MTV wasanii kutoka sehemu mbalimbali nje ya Tanzania wanatarajiwa wasili jijini Dar es Salaam siku ya kesho kwa ajili ya maandalizi ya sherehe hiyo itakayo fanyika Club Bilicanas.
Wasanii watakao wasili siku ya kesho ni pamoja na Diamond aliyekua Uingereza, Proffesor (Afrika Kusini), Sauti Sol na Amani kutoka Kenya na Radio na weasel wa Uganda ambao wanatarajiwa kupanda jukwaani siku ya Ijumaa ya tarehe 16 Mei ndani ya ukumbi wa club Bilicanas. Mbali na wasanii hao pia DJ Tira kutoka Afrika Kusini ambae pia ni DJ wa kituo cha Television cha MTV Base nae anatarajia kutua hiyo kesho.
No comments:
Post a Comment