BUKOBA SPORTS

Tuesday, May 27, 2014

UHAMISHO ENGLAND 2014: MAN UNITED KWENYE MBIO ZA KUSAJILI MAJEMBE! JORDY CLASIE, BRUNO MARTINS INDI, BASTIAN SCHWEINSTEIGER, ADAN LALLANA, THOMAS MULLER, MARCO REUS, EDINSON CAVAN

 Schweinsteiger kujiunga na kocha Louis van Gaal?
Meneja mpya wa Manchester United Louis van Gaal hana nia ya Toni Kroos wa Bayern Munich na Cesc Fabregas na badala yake anawataka Wachezaji wa Uholanzi ambayo ndie Kocha wa Timu ya Taifa.

Akiwa Kambini pamoja na Timu ya Holland inayojitayarisha kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia zinazoanza huko Brazil hapo Juni 12, imedaiwa Louis van Gaal anataka kuwachukua Wachezaji wawili walioko Kambini humo wanaochezea Klabu ya Feyenoord, Jordy Clasie and Bruno Martins Indi, ili wajiunge nae Old Trafford mara baada ya Kombe la Dunia.
Pamoja na hao, pia inasemekana LVG anamtaka Mchezaji wa AS Roma, Kevin Strootman, licha ya kuwa sasa yupo muda mrefu nje ya Uwanja akiuguza Goti lake badala ya Kiungo wa Barcelona, Cesc Fabregas.
Watatu hao, Clasie, Indi na Strootman, ni Waholanzi wenye sifa kemkem za umahiri mkubwa kiasi ambacho LVG sasa ameuagiza Uongozi wa Man United uanze mazungumzo Klabu zao na kumaliza kazi ya Uhamisho wao kimya kimya ili isije ikaonekana kama yeye, ambae ni Kocha wa Uholanzi, ametia mkono wake.

Indi na Clasie, wote wakiwa na Miaka 22 kila mmoja, wamejipatia sifa kubwa Klabuni kwao Feyenoord kiasi ambacho Clasie Msimu huu amelazimika kuchukuliwa Timu ya Taifa ya Holland na pia Nahodha wa Holland, Robin van Persie, ambae pia ni Mchezaji wa Man United, kukiri Clasie ni Paul Scholes mpya.
Nae Bruno Martins Indi, Sentahafu Mrefu, mwenye nguvu na akili, ni nguzo imara ya Feyenoord na Holland.
Jordy Clasie

No comments:

Post a Comment