Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions - Mtwara
Shindano la Kusaka VIpaji vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents limemalizika jana kanda ya Kusini, Mkoani Mtwara kwa washindi watatu kupatikana na kupewa zawadi zao za Shilingi laki tano Kila Mmoja.
Historia ilijirusia hapo jana mara baada ya Mtoto mdogo kuliko wote mwenye umri wa miaka 14 kuonyesha Kipaji cha Hali ya juu kuliko washiriki wote na kuweza kuibuka kuwa mmoja wa washindi watatu kutoka Kanda ya Kusini Mkoani Mtwara.
Washindi watatu waliopatikana jana Kanda ya Kusini Mkoani Mtwara wataungana na wa washindi wengine waliopatikana kutoka kanda ya Ziwa, Kanda ya kati, na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na kanda za Pwani na Kaskazini ambappo washindi wa kanda hizo mbili za Kaskazini na Pwani watapatikana kuanzia wiki ijayo ambapo washindi wote watakuwa ndani ya Nyumba ya TMT Na watapatiwa mafunzo na hatimaye kushindanishwa katika fainali kubwa itakayofanyika Mwezi wa Nane na Mshindi Mmoja kuibuka na Milioni 50 za kitanzania na Washindi Kumi bora wataweza kufanya filamu ya pamoja na kunufaika na mauzo ya filamu hiyo.
Wakiongelea Mashindano kwa kanda ya Kusini, Washiriki walisema wamevutiwa sana na shindano hilo na pia wameshukuru pia kwa shindano hilo kuletwa Mkoani Mtwara kwani Walisahaulika. Waliongezea kwa kusema kuwa Mashindano hayakuwa rahisi maana wengi wa washiriki walionyesha vipaji vya kweli katika kuigiza na Majaji walitenda haki katika Kuchagua
Baada ya Mashindano haya kumalizika Kanda ya Kusini Mkoani Mtwara sasa Zoezi linahamia Kanda ya Kaskazini Mkoani Arusha wiki hii ambapo Zoezi zima la usajili litafanyika kuanzi jumamosi ya tarehe 17 Mei 2014 ambapo pia watatafutwa washindi watatu.
Washindi hawa watatu wataungana na washindi wengine watakaopatikana katika kanda zingine katika fainali itakauofanyika Mkoani Dar Es Salaam Na mshindi kupata Zawadi kubwa ya Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.
No comments:
Post a Comment