Mwenyekiti wa kamati ya Rufani ya TFF, Wakili Julius Mutabazi Lugaziya akiongea na waandishi wa habari leo mchana
KAMATI ya rufani ya shirikisho la soka Tanzania, TFF, imetengeu maamuzi ya kamati ya uchaguzi wa klabu ya Simba sc wa kuliengua jina la mgombea wa Urais wa klabu hiyo, Micheal Richard Wambura.Mwenyekiti wa kamati hiyo, wakili Julius Luhaziya amesema mchana huu katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa TFF, jijini Dar es salaam kuwa kamati yake ilikaa juzi na jana na kufikia maamuzi ya kutengue maamuzi ya kamati ya uchaguzi ya Simba chini ya mwanasheria, Dkt. Damas Ndumbaro kwasababu klabu hiyo ilikiuka kanuni ilijiwekea yenyewe kwa mujibu wa katiba.
Lugaziya amesema kuwa uamuzi wa kumrudisha Wambura umeangali zaidi busara kwasababu Simba ilikiuka katiba yake kwa kumuacha mwanachama aliyesimamishwa kuendelea kufanya shughuli za klabu, na kama akiondolewa basi katiba na kamati ya uchaguzi vyote vitakuwa batili.
No comments:
Post a Comment