HATIMAE, Fainali za Kombe la Dunia zinaanza Leo hii huko Sao Paulo, Brazil wakati Wenyeji Brazil wataivaa Croatia katika Mechi ya Kwanza ya Kundi A itakayochezwa Arena Corinthians, au kwa Jina jingine Arena de Sao Paulo.
Kihistoria Mechi ya Ufunguzi huwa ngumu kwa Wenyeji na mara nyingi huanza vibaya kwa Sare au hata kufungwa.
Hali za Timu
Meneja wa Brazil, Luiz Felipe Scolari, anatarajiwa kuutumia Mfumo wa 4-2-3-1 lakini hamna uhakika kama Kiungo wa Chelsea, Oscar, anaweza kuanza kutokana na fomu yake kuporomoka hivi karibuni.
Lakini asipocheza Oscar, Mchezaji mwingine wa Chelsea, Willian, huenda akajaza nafasi yake.
Croatia wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa na pigo kubwa la kumkosa Mario Mandzukic ambae yuko Kifungoni baada ya kupewa Kadi Nyekundu kwenye Mechi yao ya Mchujo dhidi ya Iceland Mwezi Novemba.
Hata hivyo, Croatia wanae Eduardo, Mzaliwa wa Brazil, ambae ameungama akiwepo huenda akaimba Nyimbo za Taifa zote mbili ambazo huimbwa kabla Mechi kuanza.
Mvuto mkubwa kwa Duniani nzima ni kutaka kumwona Supastaa mdogo wa Brazil, Neymar, atachezaje na kama ataweza kurithi mikoba ya Lejendari Pele kwa kuwika kwenye Kombe la Dunia na kuipa Nchi yake Taji.
Uso kwa Uso
Brazil na Croatia zimeshawahi kukutana mara mbili na Brazil kushinda mara 1, Bao 1-0 huko Germany kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2006 kwa Bao la Kaka na kutoka Sare 1-1 Mwaka 2005 kwenye Mechi ya Kirafiki.
Takwimu za Mechi
Wakielekea Kombe la Dunia, Brazil wamekuwa wakifunga Watani wa Bao 2.58 kwa Gemu, wakifunga Bao 2 au zaidi katika Asilimia 84 ya Mechi zao..
Mashabiki wa Timu zote zinazoshiriki Kombe la Dunia 2014 wakiwa wamejipamba VIKOSI VINATARAJIWA:
Brazil (Mfumo: 4-2-3-1): Cesar; Alves, Luiz, Silva, Marcelo; Gustavo, Paulinho; Hulk, Oscar, Neymar; Fred.
Croatia (Mfumo: 4-2-3-1): Pletikosa; Srna, Lovren, Corluka, Pranjic; Vukojevic, Modric; Perisic, Rakitic, Kovacic; Olic.
Refa: Yuichi Nishimura (Japan)
RATIBA:KOMBE LA DUNIA LEO
Alhamisi 12 Juni:
Brazil v Croatia 23:00,
Ijumaa 13 Juni:
Mexico v Cameroon 19:00,
Jumanne 17 Juni:
Brazil v Mexico 22:00,
Jumatano 18 Juni:
Cameroon v Croatia 01:00,
Jumatatu 23 Juni:
Cameroon v Brazil, 23:00
Croatia v Mexico 23:00

No comments:
Post a Comment