Bondia Hassana Mlutu akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Iddi Mustafa wakati wa mpamnano wao Mlutu alishinda kwa point mpambano huo.
WACHEZAJI WA NGUMI WA KAMBI YA SINZA MAKABURINI WAKIMPIGA TAFU MWENZAO MORO BEST KUSHOTO NI SHEDRACK IGNAS NA WA PILI KUSHOTO BONDIA MUSTAFA DOTO
Bondia Mzee kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Ismail Ndende wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita mpambano uho ulimalizika kwa droo ya kufungana point .
Bondia Sako Mwaisege kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Hussein Gobiso wakati wa mchezo wao uliomalizika kwa droo ya kufungana kwa point .
Bondia Hassani Mandula kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Karim Migea wakati wa mpambano wao Mandula alishinda kwa k,o ya raundi ya pili .
Bondia Deo Samweli kushoto akipambana na Mann Issa wakati wa mpambano wao Samweeli alishinda kwa point
Msanii wa muziki wa hipop Karama Masoud 'Kala Pina' akitumbuiza katika onesho lake lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita lililoandaliwa na kikosi cha mizinga entertainment
Na Mwandishi Wetu
Mpambano wa masumbwi uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita ulioandaliwa na Kikosi cha Mizinga Entertainment ya jijini Dar es salaam
imeleta chachu kwa mabondia mbalimbali baada ya wengi wao kuikubali kampuni hiyo na kuiunga mkono kwa kila hali .Mmoja wa wasisi wa kampuni hi ambaye ni Msanii wa muziki wa hipop Karama Masoud 'Kala Pina' na Sempai Gola wameahidi kuwa bega kwa bega na mabondia mbalimbali kwa ajili ya kushiriki katika ngumi zitakazo pangwa tena hivi karibuni.
katika mchezo huo bondia Salum Msabaha alimsambalatisha Shabani Hamisi, na George Epson akipewa kichapo na Mohamed Kambuluta na Mwinyi Mzee akitoa droo na Ismail Ndende ,Rashid Mohamed alimshinda Sadiki Nuru kwa point,Hassani Mandula akimsambalatisha bila huruma bondia Karim Migea kwa K,O ya raundi ya pili na Julias Kisalawe akitoa droo na Hassan Kiwale
mpambano huo uliohudhuliwa na mashabiki lukuki ambao awajakaa kwenye viti vyao kwa ajili ya kushangilia mwanzo wa mchezo mpaka mwisho ambapo kila mmoja alifuraia kuona mchezo huo wa masumbwi kwa kushiliki vijana chipkizi wengi na wenye kuelewa nchezo wa ngumi
No comments:
Post a Comment