BUKOBA SPORTS

Thursday, June 12, 2014

WORLD CUP 2014: PAZIA KUFUNGULIWA LEO HII ALHAMIS USIKU KATI YA WENYEJI... BRAZIL v CROATIA


Macho ya walimwengu na wapenzi wa soko dunia hii leo yanaelekezwa nchini Brazil ambako masaa machache yamesalia hadi kuanza mashindano ya Kombe la Dunia katika mchezo wa soka.
Mechi ya ufunguzi wa mashindano hayo yanayozikutanisha timu za mpira wa miguu kutoka nchi 32 duniani, itatanguliwa na hafla za ufunguzi zitakazofanyika katika mji wa Sao Paul ambazo zinaenzi mazingira, watu na mpira wa miguu.
People wearing Brazilian flags arrive at the Santa Cruz Stadium in Ribeirao Prato on 10 June 2014
Serikali ya Brazil inatumia jeshi la anga, askari polisi na wanajeshi 147,000 kuimarisha usalama huku shule za nchi hiyo zikifungwa wakati huu wa mashindano hayo. Mechi ya ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Dunia katika mchezo wa soka itafanyika katika uwanja wa Itaquerao kati ya mwenyeji Brazil na Croatia.
Brazilian President Dilma Rousseff defended the $11 billion invested into World Cup infrastructure throughout the country, and urged people living in host cities to give a 'warm welcome' to incoming tourists, in a televised address and on social media Tuesday.
Hayo yanajiri huku kukishuhudiwa migomo na malalamiko ya wananchi ambapo Rais Dilma Rousseff wa Brazil ametetea uamuzi wa serikali yake wa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo, na kutupilia mbali madai kwamba wametumia gharama kubwa kuanda mashindano hayo. 
Ametangaza kuwa matayarisho yamekamilika na kusisitiza kuwa uwekezaji katika ujenzi wa viwanja vya mpira, viwanja vya ndege na miundombinu mingine utaipa nchi hiyo faida za muda mrefu. Rais wa Brazil pia amewataka wananchi wa nchi hiyo ya Amerika ya Latin kuunga mkono timu ya taifa hilo na kuwakirimu wageni na watalii.

No comments:

Post a Comment