Griezmann, alietamba huko Brazil akiwa na France kwenye Fainali za Kombe la Dunia na Msimu iliopita kuifungia Real Sociedad Bao 16, alikuwa pia akisakwa na Meneja mpya wa Tottenham, Mauricio Pochettino.
Lakini ni wazi sasa Atletico wameshinda mbio za kumpata Winga huyo baada Klabu zote mbili za La Liga kutoa matamko kwenye Tovuti zao wakibariki Uhmisho huo.
Atletico wao walisema makubaliano na Real Sociedad yamefikiwa baada ya wao kuweza kutimiza Dau la Kipengele cha Mfaransa huyo ambalo hubidi lilipwe ili kumruhusu ahame kabla muda wa Mkataba wake kumalizika.
Klabu hizo zimetamka kuwa Uhamisho huo utakamilika mara baada Griezmann kufuzu upimwaji afya yake huko Atletico.
Antoine Griezmann alianza kucheza na Klabu za Vijana za EC Macon Mwaka 1997 hadi 1999 kisha kwenda Timu ya Vijana ya UF Maconnais na kuhamia Timu ya Vijana ya Real Sociedad 2005 hadi 2009 alipoanza kuchezea Kikosi cha Kwanza na kucheza Mechi 179 na kufunga Bao 49.
No comments:
Post a Comment