Romelu Lukaku atakamilisha uhamisho wa kujiunga na Everton kwa dau la paundi milioni 24 baada ya kutangaza kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twita mchana wa leo akisema: Ni muda wa kuanza ukurasa mpya.
Inafahamika kuwa nyota huyo mwenye miaka 21, ambaye msimu uliopita alikipiga Goodison Park kwa mkopo atasaini mkataba wa miaka mitano na Everton na kuvunja rekodi ya usajili ya klabu hiyo.Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji aliyeiwakilisha nchi yake katika fainali za mwaka huu za kombe la dunia nchini Brazil, amekuwa akihusishwa kuondoka darajani majira yote ya kiangazi mwaka huu.Everton ameamua kumpa mkataba wa kudumu baada ya kuwa na rekodi nzuri ya kufunga mabao 15 msimu uliopita.
Kocha wa Everton Roberto Martinez akimsifia Lukaku mbele ya Waandishi wa Habari na kudai kuwa Lukaku ataonesha picha wapi wanaelekea zaidi..
Lukaku aliwachezea Everton kwa mkopo msimu uliopita na kufunga mabao kadhaa
Romelu Lukaku moja kwa moja alinaswa kwa £28million kutoka Chelsea
Lukakuna meneja wake Roberto Martinez
Matabasamu ya nguvu: Lukaku kwenye ukumbi wa Habari
Romelu Lukaku ameweka Historia kusajiliwa na Everton kwa kiasi hicho na akitokea Chelsea....

No comments:
Post a Comment