BUKOBA SPORTS

Saturday, July 26, 2014

USAJILI: KLABU YA ARSENAL YAMSAJILI CALUM CHAMBERS KUTOKA SOUTHAMPTON

Beki wa Southampton Calum Chambers amesaini kuchezea Arsenal kwa Dau la Pauni Milioni 16.
Jana Mchezaji huyo mwenye Miaka 19 anaechezea Timu ya Vijana ya England ya chini ya Miaka 19 alifanyiwa upimwaji afya yake.
Chambers anakuwa Mchezaji wa Tatu kusainiwa na Arsenal baada ya pia kuwanasa Fowadi wa Barcelona Alexis Sanchez na Beki wa Newcastle Mathieu Debuchy.
Hadi sasa Southampton imeshawapoteza Rickie Lambert na Adam Lallana waliokwenda Liverpool na Luke Shaw aliekwenda Man United.
Calum Chambers
Dili la Chambers kuja Arsenal linaangaza Carl Jenkinson kuondoka Klabuni hapo.

Bacary Sagna alishatimukia Manchester City

No comments:

Post a Comment