BUKOBA SPORTS

Friday, August 15, 2014

UEFA YATAJA WATATU KUWANIA ‘MCHEZAJI BORA ULAYA!’ LIONEL MESSI NJE! MSHINDI KUTANGAZWA AGOSTI 28.


UEFA Leo imetoa Majina Matatu ya Wagombea Tuzo yao ya Mchezaji Bora wa Mwaka na Mshindi wake atatangazwa hapo Agosti 28 wakati wa Droo ya Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.Clinical: Cristiano Ronaldo scored a record 17 goals in last season's Champions League for Real Madrid
Majina hayo Matatu ni ya Cristiano Ronaldo, Mchezaji Bora Duniani, Kipa wa Mabingwa wa Dunia Germany, Manuel Neuer na Mchezaji mwenzake wa Klabu ya Bayern Munich anaechezea Holland, Arjen Robben
Awali Majina ya Wachezaji 35 yalipigiwa Kura na kubakia 10 na kutangazwa hapo Julai 18.
Strike: Robben won the league and cup double for Bayern Munich and scored three World Cup goals for Holland
Majina hayo 10 yamechujwa kwa Kura hii Leo na kubakisha hayo Majina Matatu yatakayopigiwa Kura ya wazi wakati wa Droo ya Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
na Mshindi kutangazwa Siku hiyo hapo Agosti 28.
Double: Cristiano Ronaldo won the Champions League and Copa del Rey for Real Madrid last seasonCristiano Ronaldo

WASHINDI WALIOPITA:
2010–11 Lionel Messi [Barcelona]
2011–12 Andrés Iniesta [Barcelona]
2012–13 Franck Ribéry [Bayern Munich]



Wapigaji Kura ya Tuzo hii ni Jopo la Wanahabari maalum toka Nchi zote Wanachama wa UEFA.
Tuzo hii ilianzisha na UEFA Mwaka 2011 ili kuziba pengo la Ballon d'Or ambayo iliunganishwa na Tuzo ya FIFA ya Mchezaji Bora Duniani na pia kuibadili ile Tuzo ya zamani ya UEFA ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Klabu.


LISTI YA WAGOMBEA 10:
-Diego Costa
-Angel Di Maria
-James Rodriguez
-Luis Suarez
-Philipp Lahm
-Thomas Muller
-Manuel Neuer
-Arjen Robben
-Cristiano Ronaldo
-Lionel Messi.

No comments:

Post a Comment