Hii ni Mechi ya pili kwa kila Timu kwenye Msimu mpya wa Ligi Kuu England baada ya Wikiendi iliyopita zote kushinda Mechi zao za kwanza.
Man City walianza Ugenini huko St James Park na kuifunga Newcastle Bao 2-0 na Liverpool kuanza kwao Anfield na kushinda kwa mbinde Bao 2-1 walipoifunga Southampton huku Bao la ushindi likifungwa mwishoni na Daniel Sturridge.
Wakati Liverpool wametumia zaidi ya Pauni Milioni 100 kuimarisha Kikosi chao kwa Wachezaji wengi wapya, Man City wao Kikosi chao kwa ujumla ni kile kile cha Msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment