BUKOBA SPORTS

Monday, August 25, 2014

KOCHA WA ATLETICO DIEGO SIMEONE AFUNGIWA MECHI 8 KWA KUKWARUZANA NA MWAMUZI

Meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone amepigwa kirungu kizito na Shirikisho la Soka Spain, RFEF, kwa kufungiwa Mechi 8 baada ya kukwaruzana na Refa wa Akiba wakati wa Mechi ya Marudiano ya Fainali Supercopa de Espana dhidi ya Real Madrid Uwanjani Vicente Calderon Ijumaa iliyopita.
Diego Simeone alikwaruzana na Refa wa Akiba na mara mbili alionekana akimgonga Refa huyo nyuma ya Kichwa na Refa wa Mechi hiyo aliamua kumtoa Kocha huyo wa Mabingwa hao wa Spain.
Lakini Simeone hakutoka Uwanjani na kwenda Vyumba vya Kubadili Jezi kama huko Spain wanavyotaka bali aliamua kukaa Jukwaani akiangalia Mechi hiyo ambayo Timu yake iliifunga Real 1-0 na kutwaa Supercopa de Espana.
Matukio hayo yameifanya Kamati ya Mashindano ya RFEF imchukulie hatua kali na kumwadhibu kwa kumfungia Mechi 8 ambazo hapaswi kukaa Benchi la Ufundi wala kuwasiliana na Timu yake wakati wa Mechi hizo 8.

No comments:

Post a Comment