BUKOBA SPORTS

Saturday, August 16, 2014

ARSENAL 2 vs 1 CRYSTAL PALACE, AARON RAMSEY AIPA USHINDI GUNNERS KATIKA DAKIKA ZA MAJERUHI!

Mchezaji wa Arsenal Aaron Ramsey akishangilia bao lake baada ya kuilaza Crystal Palace kwenye dakika za majeruhi baada ya Kona kupigwa na Mabeki wa Crystal Palace kujichanganya na hatimae mpira kumkuta Aaron Ramsey na kuumalizia langoni mwa lango la Crystal Place.
Koscielny akipongezana na  Santi Cazorla baada ya kusawazisha bao katika dakika ya 45 kipindi cha kwanza.
Dakika za majeruhi za kipindi cha pili zikiwa zimeongezwa dakika 5 na Crystal Palace wakiwa pungufu, Mchezaji Aaron Ramsey aliwapa ushindi kwa kuwafungia bao na kufanya 2-1 dhidi ya Crystal Palace na Mtanange kumalizika Arsenal wakiwa na Ushindi huo wa bao 2-1 na kukwea kileleni mwa Ligi hiyo iliyoanza kutimua Vumbi leo hii jumamosi. Brede Hangeland wa Crystal Palace alivyowafunga Arsenal
Wachezaji wa  Crystal Palace wakipongezana baada ya kupata bao dhidi ya  Arsenal
Laurent Koscielny wa Arsenal alisawazisha katika dakika za majeruhi za kipindi cha kwanza.

VIKOSI:
Arsenal:
Szczesny, Debuchy, Chambers, Koscielny, Gibbs, Wilshere, Arteta, Sanchez, Ramsey, Cazorla, Sanogo.
Akiba: Rosicky, Giroud, Oxlade-Chamberlain, Monreal, Martinez, Campbell, Coquelin.
Goli: Koscielny 45+1.  Aaron Ramsey 90+1.

Crystal Palace: Speroni, Kelly, Dann, Hangeland, Ward, Puncheon, Jedinak, Ledley, Bolasie, Chamakh, Campbell.
Akiba: McCarthy, O'Keefe, Hennessey, Gayle, Murray, Bannan, Delaney.
Goli: Hangeland 35.
Refa: Jon Moss

No comments:

Post a Comment