BUKOBA SPORTS

Saturday, August 16, 2014

WEST HAM 0 vs 1 TOTTENHAM, ERIC DIER AIPA USHINDI SPURS KATIKA DAKIKA ZA LALA SALAMA WAKIWA MTU 10 KILA TIMU!!

Tottenham wameshinda Ugenini kwa Bao 1-0 walipocheza na West Ham na kila Timu kumaliza ikiwa Mtu 10.
West Ham United's Mark Noble challenges Tottenham Hotspur's goalkeeper Hugo Lloris
Tootenham walikuwa wa kwanza kumpoteza Fulbeki wao Kyle Naughton alietolewa kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 30 na Refa Chris Foy kwa kushika Mpira na pia kuwapa Penati West Ham lakini Mark Noble alipiga nje Penati hiyo.
Kipindi cha Pili, West Ham walimpoteza Beki wao James Collins aliepewa Kadi za Njano mbili ndani ya Dakika 9 tu na kupewa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 63.
Bao la ushindi la Tottenham lilifungwa na Fulbeki Eric Dier aliemzunguka Kipa na kufunga katika Dakika ya 90.
Eric Dier akimfunga kipa wa West ham katika dakika za lala salamaWachezaji wa Spurs wakimpongeza Eric DierTottenham's Eric Dier celebrates scoring their first goal with Etienne Capoue and team matesFuraha za pongezi zikimiminika kutoka hata kwa Mashabiki wao mwishoni mwa dakika 90 za mchezo! Spurs wakifurahia Ushindi!!
VIKOSI:
West Ham:
Adrian, O'Brien, Reid, Collins, Cresswell, Noble, Drampis, Vaz Te, Nolan, Downing, Cole.
Akiba: Zarate, Demel, Diame, Jaaskelainen, Poyet, Valencia, Burke.
Sam Allardyce
Tottenham Hotspur: Lloris, Naughton, Kaboul, Dier, Rose, Bentaleb, Capoue, Lennon, Lamela, Eriksen, Adebayor.
Akiba: Soldado, Holtby, Townsend, Kane, Dawson, Friedel, Davies.
REFA: Chris Foy

No comments:

Post a Comment