BUKOBA SPORTS

Thursday, August 28, 2014

MCHAKATO WA DROO YA MAKUNDI "UEFA CHAMPIONS LEAGUE" PUNDE USIKU HUU...NI TIMU ZIPI KUZIVAA MANCHESTER CITY, ARSENAL, LIVERPOOL, NA CHELSEA?

DROO ya Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI inafanyika Leo huko Monaco na Timu 4 za England, Liverpool, Chelsea, Manchester City na Arsenal, zipo kwenye mchakato huo. Droo hii itashirikisha Timu 32, 22 zikiingizwa moja kwa moja kwenye hatua hii, wakiwemo Mabingwa Watetezi Real Madrid, na Timu 10 ni zile zilizofuzu kutoka Raundi ya Mwisho ya Mchujo ikiwa ni pamoja na Arsenal.
Timu hizi 32 zitapangwa katika Makundi 8 ya Timu 4 kila moja na Timu za Kundi moja zitacheza mtindo wa Ligi kwa Mechi za Nyumbani na Ugenini.

Timu toka Nchi moja zitabaguliwa na hivyo kutowekwa kwenye Kundi moja.
Kila Kundi litatoa Washindi Wawili kusonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Shughuli za Droo hii zitaanza Saa 12 Dakika 45 Jioni, Bongo Taimu, kwenye Ukumbi wa Grimaldi Forum huko Monaco.
Kwenye Droo hiyo Timu hizo 32 zimegawanywa katika Vyungu Vinne na kila Chungu kitatoa Timu moja ili kuunda Kundi moja.

Mgawanyo huu wa kwenye Vyungu umezingatia Ubora wa kila Timu Barani Ulaya kwa mujibu wa Listi ya UEFA na Chungu Namba 1 ndio kina Timu zenye Ubora wa juu kabisa.
Kwa Klabu za England, Chelsea na Arsenal zipo Chungu Namba 1, Man City wapo Chungu Namba 2 na Liverpool Chungu Namba 3.

Msimu uliopita, Man City walitolewa Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na FC Barcelona na Chelsea kubwagwa Nusu Fainali na Arsenal kumalizia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 wakati kwa Liverpool hii ni mara yao ta kwanza kushiriki tangu Mwaka 2009/10.View image on Twitter
Best and worst-case scenarios for the Premier League teams...
CHELSEA
Best:
Chelsea, Basle, Sporting Lisbon, Maribor
Worst: Chelsea, Paris St Germain, Ajax, Roma

ARSENAL
Best: Arsenal, Basle, Sporting, Maribor
Worst: Arsenal, PSG, Ajax, Roma

MANCHESTER CITY
Best: Benfica, Manchester City, Olympiacos, Maribor
Worst: Real Madrid, Manchester City, Ajax, Roma

LIVERPOOL
Best: Benfica, Basle, Liverpool, Maribor
Worst: Real Madrid, PSG, Liverpool, Roma ends

No comments:

Post a Comment